Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

8/25/16

Kongo yaonesha nia Bomba la Mafuta Afrika Mashariki


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichoshirikisha Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya  Demokrasia ya  Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese  na ujumbe wake, pamoja na  wataalam  kutoka Wizara ya Nishati na Madini.


Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akielezea fursa za uwekezaji kwenye sekta ya  mafuta na gesi mbele ya waandishi wa habari. Kushoto ni Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese.


Kutoka kushoto, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo na Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga wakifuatilia mada iliyokuwa inawasilishwa na Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Oil of DR Kongo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Giuseppe Ciccarelli (hayupo pichani) katika kikao hicho.


Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Oil of DR Kongo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Giuseppe Ciccarelli akisisitiza jambo katika kikao hicho.Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese  na ujumbe wake wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese (kushoto)
Picha/Habari na Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya  Demokrasia ya  Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese amesema   Serikali ya   Kongo iko  tayari kushirikiana na  serikali ya  Tanzania kwenye Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.
Lusa- Diese aliyasema hayo katika kikao kilichokutanisha  ujumbe wake na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa  Sospeter Muhongo na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na  taasisi zake kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa lengo la ziara yake lilikuwa ni Serikali ya Kongo kuomba kushiriki na kuwa sehemu  ya mradi wa bomba la mafuta  ghafi la Afrika Mashariki linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi  Tanga nchini Tanzania kutokana na kwamba sehemu  ya Kongo  ina mafuta.
Alisema kuwa nchi ya Kongo kupitia wataalam wake ipo tayari kushirikiana na  Serikali ya Tanzania  kupitia  Wizara ya Nishati na Madini ili kufanikisha mradi mkubwa wa bomba la mafuta ambalo litanufaisha nchi zote za Afrika Mashariki.
Naye Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Oil of DR Kongo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Giuseppe Ciccarelli alisema kampuni yake ina uzoefu kwenye utafiti na uchimbaji wa mafuta na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki, kampuni yake itakuwa na uwezo wa kusafirisha kuanzia mapipa 30,000 hadi 100,000 kwa siku kulingana na mahitaji.
Aliishukuru  serikali ya  Tanzania kupitia  Wizara  ya Nishati na Madini kwa kuwa tayari kushirikiana na  Kongo kwenye mradi wa bomba la mafuta na kuongeza kuwa kupitia mradi huu nchi zote kwa pamoja zitapata mapato na kukua kwa uchumi wake.
Awali akizungumza katika kikao hicho,  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na  Kongo katika mradi wa bomba la mafuta  ghafi la  Afrika Mashariki  na kuelekeza wataalam kutoka nchi zote mbili kuanza  kukutana  kuanzia sasa kwa ajili ya kujadili  mpango wa ujenzi wa bomba  hilo na kumwalika Waziri wa Mafuta wa Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese kwenye kikao cha Mawaziri wa Nishati na Madini kutoka nchi za Tanzania na  Uganda kinachotarajiwa kufanyika Tanga mapema mwezi Oktoba.
Katika hatua nyingine Profesa Muhongo alisema kuwa nchi ya Kongo  imeonesha nia kwenye utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na kuongeza kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na nchi ya Kongo kupitia kampuni  za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi  ili kuongeza kasi ya ugunduzi wa mafuta katika ziwa  hilo lenye  viashiria vya mafuta.
Aidha alisisitiza kuwa mara baada ya ugunduzi wa mafuta katika Ziwa Tanganyika, nchi za Tanzania, Kongo na Burundi zitanufaika kupitia mapato pamoja na kuongezeka kwa ajira.