8/5/16

Maalim Seif kurejea leo Nchini

 

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad 
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad leo anarejea nchini kutoka ughaibuni alikokuwa na ziara ya takribani wiki tatu huku polisi wakisema jalada la upelelezi dhidi yake lipo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP).
Kupelelezwa kwa jalada hilo kwa DPP, kunatokana na maelezo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Azam wiki mbili zilizopita kuwa uchaguzi wa Zanzibar wa Oktoba 25 mwaka jana na ule wa marudio Machi 20, ulifanyika kwa amani lakini baada ya Maalim Seif kuitisha vikao vya ndani katika maeneo mbalimbali ya Kaskazini Unguja na Pemba, aliwachochea wafuasi wake kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na ndipo matatizo yalipoanza.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Makame amesema taarifa alizonazo ni kwamba jalada hilo bado lipo kwa DPP huku akisisitiza kuwa ushahidi hauwezi kupatikana bila upelelezi.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm