8/15/16

Makonda kuwajengea Bakwata ghorofaMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kujenga ofisi za kisasa kwa ajili ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) ambazo zitagharimu Sh5 bilioni.


Uzinduzi wa jengo hilo la ghorofa tatu ambalo litajengwa kwenye makao makuu ya baraza hilo wilayani Kinondoni ulifanyika jana katika hafla iliyohudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Aboubakar Zubery, masheikh na waumini wa dini hiyo.


Akizungumza leo katika hafla hiyo Makonda alisema viongozi wa dini wana mchango mkubwa wa kuleta amani na utulivu katika nchi hii.


Alisema viongozi hao wanatakiwa kupewa heshima na hadhi kwa kuthamini mchango wao wanaotoa katika jamii.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm