Mapigano yazuka upya Sudan Kusini baina ya majeshi ya pande hasimu | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

8/14/16

Mapigano yazuka upya Sudan Kusini baina ya majeshi ya pande hasimuMapigano yamezuka baina ya pande hasimu nchini sudan kusini.

Kuna hofu kuwa Sudan kusini huenda ikatumbukia tena kwenye vita vya kiraia.

Walioshuhudia wanasema wamesikia milio ya risasi katika mji muhimu wa Yei, kusini magharibi mwa Juba, kwenye barabara inayounganisha Juba na taifa jirani la Uganda.

Vikosi vitiifu kwa naibu rais, Riek Machar, vinasema kwamba vikosi vya serikali viliwashambulia katika maeneo yao siku ya jumamosi.

Mwezi uliopita vikosi vtiifu kwa rais Salva Kiir na Riek Machar vilikabiliana mjini Juba, katika makabiliano yaliyoifanya UN kutuma walinda 400 zaidi nchini humo.

Hata hivyo Bw Kiir amesema hataruhusu Umoja wa Mataifa kuchukua udhibiti wa nchi yake na hatashirikiana tena na umoja huo.

Kila upande mara kwa mara hutupiana lawama la kuanzisha vita.

Uhasama wa kisiasa baina bwana Kiir na bwana Machar uliishia kuwa mapigano mwaka 2013.

Wawili hao walitia saini mkataba wa amani mwaka 2015, japo mapigano ya mara kwa mara yamekuwa yakiendelea baina ya pande hasimu.

Zaidi ya raia 100,000 wa Sudan kusini kwa sasa wamekimbilia katika nchi jirani kufuatia mapigano ya hivi karibuni, linasema shirika la la wakimbizi la Umoja wa Mataifa.

google+

linkedin