8/1/16

Mbowe ahojiwa kwa tuhuma za uchochezi

index 
Jeshi la Polisi nchini limemuhoji Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kwa saa 2.20 kwa tuhuma za uchochezi na kisha kuachiwa huru kwa dhamana.
Mbowe aliwasili Kituo Kikuu cha Polisi jana saa 7.05 mchana baada ya kuitwa juzi na Ofisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO).
Shughuli nyingine zilikuwa zimesimama kituoni wakati mwenyekiti huyo akihojiwa mbele ya wanasheria watatu wa Chadema; Tundu Lissu, Fred Kalonga na John Mallya.
Lissu ambaye pia anashtakiwa kwa kesi ya uchochezi, aliitaka Serikali kutoa maana ya neno “uchochezi” ili kutoa fursa kwa wapinzani kuwa nalo makini pindi watakapokuwa wanazungumza na wananchi.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts