8/3/16

Miradi shule za sekondari Mwanza kuchunguzwa
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza matumizi ya fedha za mradi wa kukarabati sekondari za Mkoa wa Mwanza zilizotolewa kwa halmashauri tangu Januari.
Akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC), Mongella ametoa siku saba kwa Takukuru kutoa taarifa ya utekelezaji wa maendeleo ya ujenzi wa miundombinu shuleni.
 Amesema haiwezekani Serikali itenge fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi, lakini viongozi waliopewa jukumu la kusimamia wanashindwa.
“Nahitaji kuona nyaraka za mikataba mbalimbali na taarifa kutoka benki zilizosainiwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo shuleni,” ameagiza Mongella.

mwananchi
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm