8/29/16

Mkameruni avunjiwa mkataba Misri baada ya vipimo kuonesha ana VVU/ Ukimwi
Mshambuliaji Samuel Nlend aliyetokea klabu ya Union Douala ya nchini kwao.

Klabu ya Ittihad Alexandria ya nchini Misri imemsitishia mkataba mshambuliaji wa Kameruni, Samuel Nlend baada ya kufeli vipimo.

Nlend mwenye umri wa miaka 21 alijiunga na klabu hio ya Ligi Kuu Misri siku tatu zilizopita kwa mkataba wa miaka 3 lakini baada ya vipimo vya afya kuonesha ana virusi vya VVU/ Ukimwi amevunjiwa mkataba wake.

Nchini Misri, mchezaji hawezi kupata kibali cha kufanya kazi endapo vipimo vya afya yake vitaonesha ana magonjwa kadhaa yaliyomo kwenye orodha maalum ikiwemo VVU/Ukimwi.

Hata hivyo klabu ya Alexandria haijafanya jambo la busara kuweka wazi matokeo ya vipimo hivyo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts