8/3/16

Mkataba kati ya mwekezaji, Kijiji cha Chole wavunjwa

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Tamisemi, George
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amevunja mkataba kati ya mwekezaji wa kigeni na Kijiji cha Chole wilayani Mafia.
Simbachawene amevunja mkataba huo jana alipotembelea kijiji hicho na kusema hakikuwa na haki ya kumiliki mali za kale na kwamba, mali zote zinamilikiwa na Serikali.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa mkataba uliovunjwa ulikuwa ukiihusu Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Company Limited inayomilikiwa na Jean Devillies, mkewe Ann na Kijiji cha Chole.
Juni mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo aliagiza kupitiwa upya kwa mkataba huo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts