8/11/16

Mkuu wa mkoa Songwe apiga marufuku Ukuta
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. 

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa amepiga marufuku mikutano na maandamano yote yatakayoratibiwa kwa utaratibu wa oparesheni Ukuta chini ya Chadema kuanzia Septemba Mosi mwaka huu katika mkoa wake akisema kipindi hiki ni cha kufanya kazi na kuhamasisha maendeleo siyo  kwa maandamano na kampeni.
Galawa amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Vwawa wilayani Mbozi huku akisisitiza kwamba wakazi wa mkoa wake wapo katika shughuli za mavuno na hawana muda wa kupoteza.
Alisema viongozi wa mkoa huo wana wajibu wa kuwalinda wananchi wafanye shughuli zao kwa amani na usalama bila bugudha wala kushawishiwa na watu wengine kuingia kwenye kwenye ajenda zao
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm