Moto wateketeza madarasa, ofisi ya mkuu wa shule | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

8/29/16

Moto wateketeza madarasa, ofisi ya mkuu wa shule

MADARASA na ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kongowe Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani, vimeteketea kwa moto pamoja na nyaraka zote zilizokuwamo ndani yake.
waziri wa elimu profesa joyce ndalichako.

Diwani wa kata hiyo, Idd Kanyallu, alisema moto huo ulioanzia katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa shule, umetekeza ofisi hiyo pamoja na nyaraka zote.

Kanyallu alisema mbali ya ofisi na nyaraka hizo, pia vyumba viwili vya madarasa vimeteketea kwa moto huo na kwamba inakadiriwa hasara iliyopatikana kufikia Sh. milioni 50.
 
Chanzo: Nipashe

google+

linkedin