Mugabe afuta ziara yake nchini Ghana | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

8/19/16

Mugabe afuta ziara yake nchini Ghana

Mugabe mwenye umri wa miaka 92, ndiye kiongozi mzee zaidi barani Afrika
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefuta ziara yake kwenda nchini Ghana kupokea tuzo la Millennium Lifetime Achievement award, kwa kuliongoza taifa hilo la kusini mwa Afrika kupata uhuru wake mwaka 1980.

Rais wa Ghana John Mahama alitarajiwa kumpa Mugabe tuzo hilo, wakati wa warsha ambayo ingefanyika katika mji mkuu wa Ghana Accra.

Mugabe mwenye umri wa miaka 92, ameingoza Zimabawe tangu ipate uhuru na ameapa kusalia madarakani hadi kifo na kukataa wito wa kumtaka ang'atuke.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kwa safari hiyo, lakini mtandao mmoja nchini Ghana unawanukuu wanadiplomasia nchini Zimbabwe wakisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana masuala ya kisiasa nchini Zimbabwe.

Mabango makubwa yalikuwa yamewekwa mjini Accra kumkaribisha Rais Mugabe na pia hotuba yake ilikuwa imesubiriwa kwa hamu.

google+

linkedin