8/8/16

POGBA KUFANYIWA VIPIMOKlabu ya Juventus ya Italia imemruhusu mshambulizi wake Paul Pogba kufanyiwa vipimo vya afya Old Trafford katika moja ya ishara kuwa huenda Manchester United imeafikiana na wakala wake kumnunua mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa likizoni Marekani baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016.
Pogba, 23, amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford kwa bei ya kuvunja rekodi ya dunia ya ununuzi wa wachezaji ya pauni milioni moja.

Pogba alichezea United mwisho dhidi ya Wolves Machi 2012
Akiwa Old Trafford Pogba alichezeshwa katika mechi 3 pekee.

United wameanza msimu kwa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City.
Juventus wataanza msimu wao Serie A wiki moja baadaye tarehe 20 Agosti.

Na hii ndio Hash tag ambayo inatrend kwenye ukurasa rasmi wa man united kwenye twitter
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm