Profesa Kitila Mkumbo awachambua marais watano | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

8/22/16

Profesa Kitila Mkumbo awachambua marais watano


Japokuwa Tanzania imeongozwa na marais watano tangu uhuru, imeshindwa kuimarisha taasisi za kidemokrasia na kwamba hali ya kisiasa na ya kisera ya nchi imekuwa ikiakisi na kuchukua taswira ya kiongozi aliyeko madarakani.

Kiongozi wa nchi amekuwa akichukua taswira ya nchi na pia taswira ya nchi imekuwa ikiakisi taswira ya rais katika ujenzi wa uchumi, mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa pamoja na ujenzi wa taasisi za demokrasia.

Profesa Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye amewachambua marais wa awamu zote tano, amewamwagia sifa Mwalimu Julius Nyerere na Jakaya Kikwete kwa kujitahidi kujenga taasisi za kidemokrasia.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu mwishoni mwa wiki iliyopita ofisini kwake, Profesa Kitila alisema marais wa awamu zote wana mazuri na mabaya yao lakini alibainisha kuwa tofauti na watangulizi wake, Rais Magufuli anakabiliwa na changamoto nyingi binafsi na huenda fungate yake ya kisiasa isidumu muda mrefu.

google+

linkedin