8/31/16

Raia 86 kutoka nchini Uganda wamekamatwa mkoani Kagera.Idara ya uhamiaji mkoani Kagera imefanikiwa kuwakamata watu 86 raia wa nchi jirani ya Uganda wengi wao wakiwa wakina mama na watoto wenye umri chini ya miaka 17 waliokuwa wamejificha katika maeneo mbalimbali yaliyoko kwenye kata za Hamgembe na Rwamishenye zilizoko katika manispaa ya Bukoba ambao waliingia mkoani humo kwa lengo la kutafuta kazi ndogondogo za kujikimu kimaisha.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa idara ya uhamiaji wa mkoa wa Kagera Abdallah Towo amesema idara hiyo imefanikiwa kuwanasa watu hao baada ya kupata taarifa za kiintelijensia toka kwa wananchi, ameeleza kuwa maofisa wa idara hiyo Agosti 25 mwaka huu walikamata kundi la waganda 29 na usiku wa kuamkia jana wamekamata kundi jingine la waganda 57 na kusema kwamba miongoni mwao waliokamatwa ni watoto wenye umri chini ya miaka 17 ambao ni 58, wanawake 26 na wanaume 2 na amebainisha kuwa wanaume wengine waliokuwa wameambatana na watu hao wamefanikiwa kutoroka.

Mkuu huyo wa idara ya uhamiaji amesema idara hiyo imewafikisha mahakamani watu watatu kwa tuhuma ya kuwaingiza nchini raia hao wa nchi jirani ya Uganda, amewaja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Medard Joseph Langila ambaye ni mtanzania na Steven Gad na George Mtinga ambao raia wa Uganda.

Kwa upande wao waganda hao waliokutwa kwenye ofisi za idara ya uhamiaji ambao wanaongea kiswahili kwa shida wamesema wanaingia hapa nchini kwa lengo la kutafuta vibarua hasa vya kutembeza maziwa.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts