8/5/16

RC Iringa apiga marufuku maandamao

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amepiga marufuku maandamano ya vyama vya siasa mkoani kwake akisema kitendo hicho kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Katazo la Masenza linakuja siku moja baada ya kauli kama hiyo kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ambaye naye amekipiga marufuku mikutano na maandamano yote yatakayoandaliwa chini ya mpango wa Ukuta.
Kama alivyofanya Makalla, Masenza pia ametoa agizo kwa wakuu wa wilaya, maofisa tarafa, watendaji wakata, mitaa, vijiji na vitongoji kuhakikisha maandamano ya vyama vya siasa kwenye maeneo yao hayafanyiki.
“Hivi karibuni tumesikia matamko ya viongozi wa kisiasa wakiwataka wananchi kuandamana nchi nzima Septemba Mosi mwaka huu, kwa Mkoa wa Iringa, sitaruhusu watu kuandamana, nataka wananchi wote tufanye kazi kwa bidii na nawaomba pia kuwapuuza viongozi hao wanaowataka kufanya maandamano.”

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts