8/16/16

Shule nyingine yaungua Arusha


 

 Ikiwa takribani wiki ipite tangia Shule ya sekondari Lowasa kuungua, moto umezuka tena na kuteketeza mabweni ya Shule ya Sekondari Mlangarini
Shule hiyo iliyopo Wilaya ya Arumeru, jijini Arusha imekuwa ni miongoni mwa shule 5 ambazo ndani ya mwezi moja zimeteketea kwa moto huku uchunguzi bado ukiwa bado unaendelea
Kufuatia kuwaka kwa moto na kuteketeza sehemu kubwa ya bweni la wavulana watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.
Akitaja waliokamatwa mkuu wa shule hiyo Elias Johhn Pallakyo alisema ni  walinzi wawili pamoja na walimu wawili wa zamu kwa usiku huo

-mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts