8/20/16

Simba SC Yaibuka Kidedea na Mchezo wake Dhidi ya Ndanda FC kwa Jumla ya Mabao 3 kwa 1


Klabu ya wekundu wa Msimbazi , Simba imefungua dimba la ligi kuu kwa “spidi ya 4G ” baada ya kuilaza Ndanda FC bao 1 – 0 , mechi iliyotimua vumbi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mshambuliaji hatari wa Simba , Laudit Mavugo ndio alikua wa kwanza kufungua hesabu ya magoli dakika ya 20 baada ya kumalizia vizuri mpira wa adhabu kutoka kwa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ .Dakika ya 37 , Omary Mponda wa Ndanda FC aliweza kusawazisha bao baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa nahodha wa Ndanda , Kiggi Makassy. Hadi mpira unaenda mapumziko , Simba 1 – 1 Ndanda FC .

Kipindi cha pili kilianza , huku mchezo ukiwa ni vuta nikuvute , hadi dakika ya 73 ambapo mshambuliaji mpya wa Simba kutoka Ivory Coast ambae aliingia akitokea benchi mwanzoni wa kipindi cha pili , Frederick Blagnon aliweza kuipatia Simba bao la 2 kwa kichwa kwa kumalizia kona nzuri ya Tshabalala .

Shiza Kichuya aliweza kufunga hesabu ya mabao , baada ya kuifungia Simba bao la 3 lililotokana na mpira wa Kona ambayo ilitemwa na kipa wa Ndanda FC , Jackson Chove na kumwachia mwanya Kichuya kuingiza nafasi ya kuusogeza mpira nyavuni . Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa , SImba 3 – 1 Ndanda FC .
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm