8/1/16

Simbachawene Awasimamisha kazi Maofisa Elimu Wawili Songwe na Mbeya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
Maofisa elimu wawili katika mikoa ya Songwe na Mbeya wamesimamishwa kazi baada ya wanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya  Sekondari ya Ileje kukutwa wamelala chini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene ndiye amewasimamisha vigogo hao.
Waliotumbuliwa ni Ofisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Mwalimu Charles Mwakalila na Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ileje, James Milanzi, ambao wanatuhumiwa kutoisimamia vizuri shule hiyo.
Waziri Simbachawene amesema jana kuwa ameamuru Mwalimu Mwakalila asimamishwe kwa sababu ndiye alikuwa anasimamia shule zote za mikoa ya Mbeya na Songwe wakati wanafunzi hao wanapokewa kabla ya utawala wa mikoa hiyo haujagawanywa.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts