8/17/16

Sina tatizo na Baraka The Prince- Young Killer

Rapa Young Killer anayeiwakilisha vyema Mwanza katika muziki wa Hip hop amefunguka na kusema kuwa yeye hana tofauti yoyote na msanii Baraka The Prince ambaye awali alishawahi kunukuliwa kuwa havutiwi na kazi za msanii huyo.
Rapa Young Killer
Young Killer alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio alidai kuwa yeye hana tofauti yoyote na Baraka The Prince na kusema alisikia hizo tetesi lakini yeye anamkubali Baraka The Prince kutokana na kazi zake na uimbaji wake mzuri.
"Mimi mwenyewe nilisikia hizo tetesi mtaani lakini ukweli ni kwamba sina tofauti na Baraka The Prince na mimi ninamkubali sana kazi zake nzuri pamoja na uimbaji wake mzuri, kuhusu huyo Eddu Boy naomba nisimzunguzie sababu sipo naye karibu kwa muda mrefu hivyo sijui chochote juu yake" alisema Young Killer
Mbali na hilo Young Killer amesema kuwa kwa sasa amerudia utaratibu wake wa zamani kutoa kazi kila baada ya miezi mitatu ili kuwa karibu na mashabiki zake.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm