8/12/16

Tanzania kunufaika na mpango wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ya kujenga Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Dkt. L. Chamuriho akielezea jambo wakati wa ugeni wa Mwakilishi Mkuu wa Ubalozi wa China hapa nchini Lin Zhiyong (kushoto) walipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kufanya tathmini kama kinakidhi vigezo kuwa miongoni mwa Vyuo vitano vitakavyojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kufuatia dhamira ya Rias wa nchi hiyo ya kujenga vyuo vikuu vitano vya usafirishaji barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa akifafanua jambo wakati wa ugeni wa Mwakilishi Mkuu wa Ubalozi wa China hapa nchini Lin Zhiyong (kushoto) walipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kufanya tathmini kama chuo hicho kinakidhi vigezo kuwa miongoni mwa Vyuo Vitano vitakavyojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kufuatia dhamira ya Rias wa nchi hiyo ya kujenga vyuo vikuu vitano vya usafirishaji barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Dkt. L. Chamuriho na Katibu wa Tatu wa Balozi wa China nchini Sun Chengfeng.
Mwakilishi Mkuu wa Ubalozi wa China hapa nchini Lin Zhiyong akiangalia namna mafunzo ya Urubani yanavyotolewa katika Chuo cha Taifa cha Usafirisha (NIT) walipotembelea chuoni hapo leo kwa ajili ya kufanya tathmini kama kinakidhi vigezo kuwa miongoni mwa Vyuo Vitano vitakavyojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kufuatia dhamira ya Rias wa nchi hiyo ya kujenga Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika.
Naibu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Dkt. Mhandisi Prosper Mgaya akitoa maelezo ya  mpango wa maboresho ya chuo hicho wakati wa ugeni wa Mwakilishi Mkuu wa Ubalozi wa China hapa nchini Lin Zhiyong (katikati) walipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kufanya tathmini kama chuo hicho kinakidhi vigezo kuwa miongoni mwa Vyuo Vitano vitakavyojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kufuatia dhamira ya Rias wa nchi hiyo ya kujenga vyuo vikuu vitano vya usafirishaji barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Profesa Zacharia Maganilwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Dkt. L. Chamuriho (katikati) akimkabidhi zawadi ya sanamu ya mnyama Faru Mwakilishi Mkuu wa Ubalozi wa China hapa nchini Lin Zhiyong (kushoto) kwa niaba ya Balozi wa Chinahapa nchini (hayupo pichani) walipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kufanya tathmini kama kinakidhi vigezo kuwa miongoni mwa Vyuo vitano vitakavyojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kufuatia dhamira ya Rias wa nchi hiyo ya kujenga vyuo vikuu vitano vya usafirishaji barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa chuo hicho Profesa Zacharia Maganilwa.
Picha zote na: Frank Shija.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts