Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

8/20/16

Viongozi Shinyanga watimuliwa bungeniKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), imewatimua watumishi wa Halmashauri ya Shinyanga, mbele ya Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene baada ya kushindwa kuwasilisha idadi kamili ya vitabu vilivyotakiwa kwa ajili ya ukaguzi.

Simbachawene alionesha kukasirishwa na kusema kitendo hicho kinatia mashaka kuwa huenda fedha za serikali zinatumika vibaya.

Mwenyekiti wa LAAC, Vedastus Ngombale-Mwiru aliwaambia viongozi wa halmashauri hiyo kuwa, katika taarifa zao kuna kasoro nyingi ambazo kamati haiwezi kuendelea na hoja za kuwauliza.

Viongozi wa halmashauri hiyo waliokuwepo kwenye kamati hiyo ni pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela na Naibu Meya, Agnes Machila.

Mara baada ya halmashauri hiyo kukaa kwenye chumba cha mkutano kwa ajili ya kuhojiwa, Ngombale-Mwiru aliwataka kurudi kujipanga upya kutokana na kushindwa kutoa hoja za ukaguzi.

Alisema inaonekana idadi ya vitabu vilivyowasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) havilingani na vitabu vilivyowasilishwa katika kamati hiyo. Ngombale-Mwiru alisema kulikuwa na hoja 26 katika Mwaka wa Fedha 2013/2014, lakini hazikuoneshwa katika vitabu vilivyoletwa katika kamati hiyo.

Alisema pia kuna uzembe mkubwa wa kushughulikia hoja za ukaguzi kati ya hoja 57 zilizokuwepo zilizojibiwa ni hoja 15, hivyo hoja 42 kutoshughulikiwa. Aidha alisema hoja nyingine 17 za miaka ya nyuma pia hazikushughulikiwa.

‘’Kamati imeridhisha kuwa hawampo tayari kuhojiwa, nawarudisha mkajipange upya na hesabu ya 2014/2015 tutawaita kwa uhakiki zaidi,’’ alisema.

Msovela alikiri kutokea kwa makosa hayo na kuahidi kwenda kujipanga upya na kurudi na majibu ya hoja zote.

‘’Tumepokea, tunakwenda kujirekebisha tutakuja tukiwa tumeishajirekebisha,’’ alisema.

Naye Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Machira alisema mapungufu yaliyojitokeza watakwenda kuyafanyia kazi ili kusiwe na makosa wakati wa kuwasilisha kipindi kingine.

Kwa upande wake, Simbachawene alisema tayari serikali imeshatumia gharama kubwa kuwalipia safari na kuishi Dodoma, lakini yaliyofanyika si mazuri na akaomba wakajipange upya ili kutoa majibu na kama watashindwa serikali itajenga mashaka katika uwezo wao.

Manispaa ya Shinyanga ndiko anakotoka Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulam Mkadam ambaye pia ni Meya ambaye wakati wote amekuwa mkali kwa halmashauri kuweka vizuri mahesabu yao. Gulam hakuwepo katika kikao hicho na badala yake aliwakilishwa na Machira.