8/16/16

Vyama vya siasa vyamkubali Ndugai

BARAZA la Vyama vya Siasa (TCD), limempongeza Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwa mpango wake wa kutafuta mwafaka wa mvutano wa wabunge wa upinzani na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson.
Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter Mziray.
Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter Mziray alisema katika taarifa yake jana kuwa uamuzi wa Ndugai kusaka suluhu ya mvutano huo unafaa kuungwa mkono na Watanzania wote wapenda amani.
“Kitendo cha Spika kuahidi kuunda kamati ya maridhiano ya mfano wa kamati kama hiyo wakati wa Bunge la Katiba, niseme kwamba naona anaenda kupata mwafaka wenye manufaa kwa taifa, hasa kwa kuwa Kiongozi wa Upinzani (Freeman Mbowe) naye ameafiki,” alisema.
Mziray alisema uamuzi huo ni wa busara, hasa ikizingatia kuwa hali ya kisiasa imechafuka ndani ya bunge na kuathiri shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti huyo alimshauri Spika kuunda kamati ya maridhiano yenye wajumbe wachache.
“Ili kuweka mambo vizuri Kiongozi wa Upinzani atoe nusu ya wajumbe wa kamati na upinzani umkubali huyo atakayekuwa mwenyekiti wa kamati," alisema Mziray ambaye ni mwenyekiti wa PPT-Maendeleo.
"Kwa uzoefu wangu Mwenyekiti ni lazima akubalike kwa maandishi na pande zote mbili, yaani CCM na upinzani.”
Aidha, Mziray alisisitiza kuwa mgogoro uliopo bungeni ni kati ya CCM na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hivyo akipatikana Mwenyekiti anayekubalika pande zote mzozo utamalizwa kwa muda mfupi.
Kambi rasmi ya upinzani.
Wapinzani walianza kususia vikao vya Bunge mwishoni mwa Mei mwaka huu baada ya Dk. Tulia kukataa Bunge kujadili kwa dharura sakata la kutimuliwa wanafunzi 7,802 waliokuwa wakisomea kozi maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm