Wahandisi 347 wafutiwa usajili | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

8/31/16

Wahandisi 347 wafutiwa usajili


Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) imewafutia usajili wahandisi 347 kwa makosa mbalimbali ya kimaadili katika taaluma hiyo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Msajili wa ERB, Injinia Steven Mlote amesema jana kuwa baadhi ya makosa hayo ni kusimamia kazi ambazo zilikuwa chini ya kiwango.

Injinia Mlote amesema hayo wakati akitangaza siku ya wahandisi ambayo itafanyika kesho, Septemba Mosi na Rais John Magufuli atakuwa mgeni rasmi ambako atashuhudia wahandisi 200 wakila kiapo cha utii.

“Watakula kiapo mbele ya Rais Magufuli ili kuhakikisha wanawajibika vyema kwa kufuata maadili kwenye taaluma yao,” amesema.

- Mwananchi

google+

linkedin