8/17/16

Wamachinga Mbeya wapewa siku 7 kutoka mjini


Serikali ya Mkoa wa Mbeya, imeanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kuwataka wafanyabishara wadogo maarufu kama wamachinga kuhamia maeneo maalumu yaliyotengwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla,
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla, ambapo amewaamuru machinga wote jijini humo kuondoka mara moja maeneo yasiyo rasmi ili kutekeleza kwa vitendo agizo la kuweka jiji hilo katika muonekano wa kuvutia na usafi wa kupigiwa mfano.
Mhe. Amosi Makalla amesema ametoa ilani ya siku saba kwa wafanyabiashara hao kuhamia maeneo yaliyotengwa kwa hiyari yao lakini wameonesha kukaidi agizo hilo hivyo basi itatumika nguvu kuwaondoa.
Wakizungumza wakati wakijitetea sababu za kuendelea kubaki katika maeneo hayo wamesema kuwa ni kutokana na kukosa maeneo ya kufanyia biashara zao katika maeneo hayo rasmi yaliyotengwa kwa ajili yao.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts