Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

8/20/16

Waziri Dkt. Mwakyembe azindua Chama cha Sheria za Habari Tanzania


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandhi wa habari (hawapo pichani) baada ya kuzindua Chama cha Sheria za Bahari Tanzania kwenye ukumbi wa Chuo cha Bahari (DMI) leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Chama cha Sheria za Bahari Tanzania Nahodha Ibrahim Bendera, akizungumza baada ya uzinduzi wa chama hicho uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Makamu wa Rais Bara wa chama hicho Dkt. Tumaini Gurumo.
 Rais wa Chama cha Sheria za Bahari Tanzania, Prof. Costa Mahalu akichangia jambo kwenye kikao cha chama hicho ambacho kilimchagua kushika wadhifa huo, kilichofanyika baada ya uzinduzi wa chama leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Wakili Ernest Mbuli na Mweka Hazina Wakili Donald Chidowu.
  Wakili Bernard Mbakileki akieleza jambo kwenye mkutano wa Chama cha Sheria za Bahari Tanzania.Kulia kwake ni Makamu wa Rais Zanzibar wa chama hicho na Wakili Salim Mnkonje na kushoto  kwake ni Wakili Mashaka Mfala.
 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiagana na Prof. Costa Mahalu baada ya uzinduzi wa Chama cha Sheria za Habari Tanzania ambacho kimemchagua  Prof. Mahalu kuwa Rais wake.Kushoto ni Wakili Donald Chidowu.
Mwenyekiti wa Chama cha Sheria za Bahari Tanzania Prof. Costa Mahalu (katikati) akiongoza kikao cha chama hicho baada ya uchaguzi uliofanyika baada ya uzinduzi wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.Kulia kwake ni Katibu wa chama Nahodha Ibrahim Bendera na Makamu wa Rais Zanzibar Wakili Salim Mnkonje wakati kushoto ni Mweka Hazina Wakli Donald Chidowu na Makamu wa Rais Bara wa chama Dkt. Tumaini Gurumo.

Picha na Hussein Makame