8/17/16

Young Killer: Anayetaka Kuniandikia Wimbo Aje


Rapa kutokea Mwanza Young Killer amefunguka na kudai kuwa kwa sasa amefungua milango kwa Mwandishi yeyote anayeweza na kutaka kumwandikia wimbo.
Akiongea na Times Fm, Killer amedai kwa sasa ni muda muafaka kwa kuwa hakuwahi kuandikiwa nyimbo hapo kabla na Mashabiki wameshaufahamu uwezo wake mkubwa alionao kwenye sanaaa.
“Nishaonyesha uwezo mkubwa na siku wahi kuandikiwa nyimbo hata siku moja toka nimeanza, sasa nafungua dirisha la usajili kwa yeyote anayetaka kuniandikia ngoma” Alisema.
Katika hatua nyingine rapa huyo amedai tayari amekwasha waandikia nyimbo wasanii wengi wakubwa kwa wadogo ila hayupo tayari kuwataja kulingana na alichokiita ‘FITINA’ katika muziki.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts