9/11/16

Abiria azua kizaazaa uwanja wa ndege Dar


ABIRIA mmoja wa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, amezua kizaazaa na kusababisha ndege kuchelewa kuondoka katika Uwaja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.Ndege hiyo ilikuwa imekaa uelekeo wa kuanza kupaa kwenye njia yake na ndipo wahudumu wakashtuka kuona mmoja wa abiria hakuwa kwenye kiti chake kwa muda mrefu.

Taarifa ambazo Nipashe ilizipata zilisema ndege hiyo aina ya Boeing ilikuwa inajiandaa kupaa jana jioni kwenda Addis Ababa, Ethiopia.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wahudumu hao walipatwa na wasiwasi na kuwaarifu marubani kabla ndege hiyo kuanza kupaa na kisha kuanzisha msako kujua aliko abiria huyo.
 
NIPASHE
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts