9/18/16

Aliyebaka na kulawiti kwenye kaburi afungwa miaka 30 jela


 
 Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemhukumu Ally Rashid  maarufu ‘Ally Mwizi’ kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka na kumlawiti mwanamke wa miaka 25 kwenye kaburi.
Hakimu Chiganga Ntengwa alitoa hukumu hiyo juzi baada  ya mahakama kuridhishwa na ushahidi  wa upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali Mkoa wa Katavi, Jamila Mziray.
Hakimu  Ntengwa  alisema amemhukumu mshtakiwa huyo baada ya kumtia hatiani kwa mujibu wa  Kifungu cha Sheria   Namba 154 ya adhabu sura namba 16.
Alisema hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa mshtakiwa huyo ili akitoka  gerezani awe  na tabia   njema  kwenye jamii.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm