9/17/16

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni Christopher Bageni Ahukumiwa Kunyongwa

 Image result for Christopher Bageni
Mahakama ya Rufaa imemtia hatiani aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni na kumhukumu kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara wanne na dereva taxi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Katika rufaa hiyo, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maafisa wengine wawili wameachiwa baada ya kushinda rufani hiyo dhidi yao ambapo mahakama hiyo imeona hakuna ushahidi wa wazi ama mazingira kuwatia hatiani.
Akisoma hukumu hiyo msajili wa mahakama ya rufaa John Kayoza amesema hukumu hiyo imetokana na rufaa iliyokatwa na DPP dhidi ya hukumu iliyotolewa na mahakama kuu iliyowaachia huru washtakiwa wa kesi hiyo.
Katika kesi ya msingi, Bageni alidaiwa kuwaua kwa kukusudia wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, aliyekuwa dereva wa teksi wa Manzese , Januari 14, mwaka 2006, katika msitu wa Pande Mbezi Luis
Katika hatua nyingine aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA DICKSON MAIMU na wenzake leo wamefanikiwa kupata dhamana ambayo hata hivyo ina masharti kadhaa ikiwemo fedha taslimu au mali isiyohamishika.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts