9/11/16

Amuua Mwezake kwa Kugombania "Sola"
RPC wa Geita, Isack Msengi
RPC wa Geita, Isack Msengi 

Geita. Mkazi wa Kijiji cha Nkome, wilayani hapa amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumuua Neema Daniel (24) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali wakati wakigombania sola.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Issack Msengi amesema umeme huo wa sola ulikuwa umeazimwa na Daniel, hivyo mtuhumiwa alipokuwa anadai kurudishiwa ndiyo kukatokea ugomvi.
Msengi amesema mtuhumiwa alimchoma Daniel na kitu chenye ncha kali kifuani na kufariki dunia papo hapo.
Kamanda huyo amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani baada ya kuhojiwa na polisi.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts