Asilimia 58 ya watanzania hawampingi Magufuli | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

9/15/16

Asilimia 58 ya watanzania hawampingi Magufuli

Utafiti mpya umebaini kuwa asilimia 96 ya wananchi wanamkubali Rais John Pombe Magufuli.

Taasisi ya Twaweza jana ilitoa utafiti huo ambao ulibaini zaidi kuwa asilimia 58 ya wananchi hao hawapingia kitendo chochote cha Rais.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye utafiti uitwao Rais wa Watu? Tathmini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya tano. Muhtasari huu unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi.

Utafiti huo ni wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.


Twaweza walieleza kuwa matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,813 kutoka maeneo yote Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 4 Juni na tarehe 20 Juni 2016.

Mengine yaliyofanyiwa utafiti ni pamoja na uondoaji wa wafanyakazi hewa ulitajwa na asilimia 69 ya wananchi wa Tanzania, kama juhudi mojawapo ya Rais John Pombe Magufuli, wanayoifurahia sana.

Elimu bure (asilimia 67) na usimamishwaji wa watumishi wa serikali (asilimia 61) navyo pia vilishika nafasi za juu. Walipoambiwa wataje vitendo ambavyo hawakubaliani navyo, asilimia 32 walitaja kuzuiliwa kwa uagizwaji wa sukari na bei elekezi ya sukari.Pamoja na hayo, asilimia 88 ya wananchi wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo, mpaka mwisho wa awamu yake ya uongozi.
Viwango vya kukubalika vya viongozi wengine wa serikali pia vipo juu Wananchi wanaonekana kumkubali mwenyekiti wao wa kijiji/mtaa (asilimia 78), diwani wao (asilimia 74) na mbunge wao (asilimia 68).

google+

linkedin