9/2/16

Bodaboda wapewa mwezi kuacha kudeka


Waendesha pikipiki (bodaboda wakiwa kwenye
Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) Mkoa wa Pwani, kwa kushirikiana  na Halmashauri ya Mji Kibaha, imewapa mwezi mmoja kuanzia juzi wamiliki wa pikipiki na bajaji kukata leseni ya usafirishaji abiria.
Agizo hilo lilitolewa jana kwenye kikao kilichowakutanisha waendasha pikipiki za abiria, uongozi wa halmashauri, Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani na Sumatra.
Ofisa Leseni wa Sumatra Mkoa wa Pwani, Mwasi Christian alisema kinachofanyika ni utekelezaji wa sheria inayoeleza umuhimu wa leseni ya usafirishaji abiria.
Hata hivyo, waendesha  bodaboda  walisema muda wa mwezi mmoja waliopewa ni mfupi na kuomba kuongezewa miezi mitatu, ombi hilo lilipingwa na Sumatra.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm