9/15/16

Bodi ya mikopo yapanga kutumia mitandao ya simu kukusanya madeni.
Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini imesema inatarajia kuanza kutumia mitandao ya simu kukusanya fedha kwa walionufaika na mikopo ya bodi hiyo huku ikisema pia itatumia mamlaka za kisheria kuhakikisha kila aliyenufaika na mikopo anarejesha tena kwa wakati.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na minong’ono ya watu kudai kupachikwa madeni na bodi hiyo ya mikopo huku wao wakiwa si walionufaika na mikopo, zaidi walalamikaji 200 wamekwisha kuwasilisha malalamiko yao mbele ya bodi ingawa hadi sasa watu 10 hadi 15 hufika na malalamiko ya kubambikiwa deni la mkopo ambapo sasa bodi inakiri kwamba tatizo ilikuwa ni mfumo.

Ameiambia ITV, katika mahojaino hayo kuwa bodi kwa sasa imekwisha kukopesha zaidi ya trilioni 2.4, ambapo fedha zilizo tayari kwa ajili ya kukusanywa zikiwa ni bilioni 284, ambapo licha ya kuanza kukusanya fedha hizo kupitia mitandao ya simu wanatarajia kubadili sheria ya mikopo ambayo itamlazimu mwajili kumkata mfanyakazi wake asilimia 15 tofauti na asilimia 8 ya awali ili kurahisisha urejeshwaji wa mikopo hiyo.
Mkurugenzi huyo mtendaji wa bodi ya mikopo amewataka waajiri wote nchini kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa wa bodi ambao sasa wameanza kupeleka taarifa za wadaiwa wa mikopo, huku akiahidi kuanza kutumia taarifa zilizoko katika taarisi kama brela, mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha hakuna mnufaika yeyote atakayesalia bila kurejesha fedha alizokopeshwa.
chanzo: ITV
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm