9/1/16

Bosi Nida Augua Gerezani

MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu, jana hakufikishwa mahakamani kwa ajili ya kesi yake iliyotajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, huku zikiwapo taarifa zisizo rasmi kuwa ni mgonjwa.
Maimu na wenzake wanane, wanakabiliwa na mashtaka ya kuhujumu uchumi ikiwamo kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh. milioni 901.
Kesi hiyo ya msingi ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, aliyepangiwa usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo kuwa na udhuru.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts