Chuo cha NIT wazindua mafunzo ya urubani | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

9/21/16

Chuo cha NIT wazindua mafunzo ya urubani


CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) nchini wameandika historia kwa mara ya kwanza tangu kianzishwe miaka 40 iliyopita baada ya kuzindua mafunzo ya urubani.
Mafunzo hayo yalizinduliwa chuoni Dar es salaam jana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa aliyekitaka chuo hicho kutoa marubani waadilifu.
Alisema Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya marubani ambapo Serikali ilihangaika kupata marubani waadilifu baada ya kulifufua Shirika la Ndege nchini (ATCL).
Aliongeza kuwa, Serikali ipo tayari kukijengea uwezo chuo hicho ili kiweze kutoa wataalamu wazuri wenye uzalendo na uadilifu kwani hao ni sababu ya Tanzania kutokuwa na marubani waadilifu.
“Serikali iko tayari kukisaidia chuo hiki ila naomba mnihakikishie kama mtatoa marubani wazuri wenye sifa
ya uadilifu kulingana na soko la ajira,” alisema.
Prof. Mbarawa alisema hakuna sababu ya kutoa marubani ambao hawakubaliki kwenye soko la ajira ambapo jambo hilo likitokea hakuna sababu ya uwepo wa chuo hicho.
Mkuu wa chuo hicho, Dkt. Zacharia Mganilwa, alisema mafunzo hayo yatatolewa na marubani waliobobea katika taaluma hiyo. “Wakufunzi wetu ni marubani ambao wapo kazini hivyo watatumia muda wa ziada kuja kutoa mafunzo kwa marubani wanafunzi, chuo kimenunua kifaa maalumu cha kufundishia marubani ili waweze kuwa mahili baada ya kuhitimu
masomo yao,” alisema.
Alisema mafunzo hayo ya wiki mbili hadi tatu yatawawezesha wakufunzi kufundisha wanafunzi wanaosomea urubani kabla ya kurusha ndege wani mtu anayesomea masomo ya urubani kwa mwaka mmoja kabla ya
kuanza kurusha ndege lazima ajifunze kwa kutumia kifaa hicho.
Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa, alisema ndege mbili mpya zilizonunuliwa na Serikali zitawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kati ya Septemba 19 na 25, mwaka huu, zikitokea nchini Canada.
Alisema ndege ya kwanza itafika nchini Septemba 19, yapili Septemba 25, mwaka huu ambapo Serikali itatangaza tenda ya ununuzi wa ndege nyingine mbili aina ya Jet.
“Serikali imenunua ndege hizi kulingana na jiografia ya viwanja vya ndege nchini, asilimia kubwa ya viwanja hivyo haviwezi kutumika na ndege kubwa…ndege hizi zitafanya safari za ndani hivyo Watanzania hawana budi kuzitumia,” alisema.
“Wakufunzi wetu ni marubani ambao wapo kazini, hivyo watatumia muda wa ziada kuja kutoa mafunzo kwa marubani wanafunzi”
Dkt. Zacharia Mganilwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)

chanzo: Majira

google+

linkedin