9/27/16

CUF Yamtimua Uanachama Lipumba


Baraza Kuu la chama cha CUF limemtimua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuanzia leo.


Katika kikao chake kilichoongozwa na Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed Katani kimepitisha uamuzi huo leo baada ya kuungwa mkono na wajumbe wote 43 waliohudhuria kikao hicho.


Mashtaka dhidi ya Limba yaliandaliwa na Sekretarieti ya chama yakimtuhumu kufanya vurugu, kuharibu mali za chama na kudharau barua ya wito wa chama kwenda kujitetea.


Mwishoni mwa wiki Lipumba aliongoza mashabiki wake kuvunja geti na milango ya ofisi ya chama hicho, Buguruni Dar es Salaam baada ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu, hatua iliyoungwa mkono na Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi.

chanzo: Mwananchi
Share:
Post a Comment

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts