9/17/16

CWT yawazuia walimu kushiriki mkesha wa Mwenge wa Uhuru
. Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa Shinyanga, kimewazuia walimu kushiriki mkesha wa Mwenge wa Uhuru kwa kulazimishwa, huku washiriki wengine kutoka halmashauri na Serikali Kuu wakishiriki kwa kulipwa posho.

Hayo yamekuja siku chache baada ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Deogratius Kapami kuwataka walimu wote kushiriki mkesha huo na ambaye hatashiriki atachukuliwa hatua.

Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga, George Nyangusu alisema hayo wakati akifungua mkutano wa walimu wa Halmashauri ya Mji Kahama, Msalala na Ushetu ambao uliitishwa kwa ajili ya utambulisho wa benki ya walimu.

Nyangusu alisema ushiriki wa mkesha huo ni wa hiyari, tofauti na baadhi ya halmashauri ambazo hutumia nguvu ya mwajiri kuwalazimisha walimu kushiriki.

Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Kahama, Victor Tandise alisema benki hiyo itapunguza matatizo ya walimu kiuchumi, huku akivitaka vikao vya juu kuangalia changamoto zinazoikabili kwa umakini.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts