9/17/16

Dodoma kuongezewa huduma za matibabu
Serikali imepanga kuongeza huduma za matibabu mkoani hapa baada ya kufanya uhakiki wa uhaba wa madaktari bingwa uliopo Hospitali ya Figo ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuongeza idadi ya wataalamu hao.

Akifunga mafunzo ya wadadisi wa utafiti wa vichocheo vya Ukimwi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) hivi karibuni, Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema hospitali hiyo ya kisasa ni maalumu kwa matibabu ya ugonjwa wa figo, lazima iwe na madaktari wa kutosha.

“Mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma na katibu wangu mkutane kuangalia ni madaktari bingwa wa aina gani wanakosekana ili tuwalete kwa sababu tunataka kuifanya Dodoma kuwa kitovu cha matibabu nchini,” alisema.

Aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na Japan imeleta mitambo maalumu ya kupimia magonjwa ya figo, moyo na saratani ya matiti, ambayo imefungwa katika hospitalini hapo.
chanzo: Mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts