9/7/16

Hawajasoma Sayansi Tangu JanuariSerengeti. Wakati Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ikiagiza wanafunzi wasome masomo ya sayansi, wa kidato cha tatu na cha nne katika Shule ya Sekondari ya Ring’wani wilayani hapa Mkoa wa Mara, hawajafundishwa masomo hayo tangu Januari mwaka huu kutokana na ukosefu wa walimu.

Wakizungumza katika mafunzo ya afya ya uzazi yaliyoratibiwa na asasi ya Girls Education Support Initiatives (Gesi) shuleni hapo wanafunzi hao wamesema licha ya kukosa masomo hayo baadhi yao wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka huu.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu, Evelyne Carlos amesema baadhi yao wamelazimika kubadili mikondo baada ya kukosa walimu hao kwa takribani mwaka mmoja.

Ofisa Elimu Taaluma, Shule za Sekondari Wilaya ya Serengeti, Jane Mwakalinga alithibitisha kuwa ana upungufu wa walimu wa sayansi 146 .
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts