9/20/16

Hoteli yafungiwa, 25 hatarini kupoteza ajira


WAFANYAKAZI 25 wa hoteli ya Obama Beach Bungalouws wapo katika hatari ya ya kupoteza ajira baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Vuai Mwinyi Mohamed, kuifungia kutoa huduma ya vinywaji na muziki kwa muda usiyojulikana.
Akizungumza na Nipashe jana, Meneja wa hoteli hiyo, Peter Sipano, alisema hoteli yake iliyopo Kiwengwa Gulioni, imefungiwa kutoa huduma za vinywaji, chakula na pamoja na burudani ya muziki tangu Septemba 7, mwaka huu.
Alisema amri ya kutakiwa kufunga huduma waliipokea kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kaskazini B kupitia barua nyenye kumbukumbu namba HW/KASK.B/M.42/VOL.11/96.
“Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya Kaskazin B Unguja imepokea agizo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kaskazini B kwamba kuanzia tarehe ya barua hii unafungiwa uuzaji wa baa pamoja na kupiga muziki,”imesisitiza barua hiyo na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Hamada Kheir.
Sipano alisema wamekuwa wakitoa huduma za vinwaji na muziki kwa muda wa miaka 9tisa tangu kuanzishwa kitega uchumi hicho pamoja na huduma za kulaza wageni wakiwamo watalii.
Alisema mkasa wa kufungiwa kutoa huduma za vinwaji na muziki umekuja akiwa tayari amelipa leseni ya vileo ya mwaka Sh. milioni 1.5 na kibali cha muziki Sh. 500,000 katika Baraza la Sanaa na Muziki pamoja na kupewa leseni ya mradi na Kamisheni ya Utalii Zanzibar.
Hata hivyo alisema baada ya kufuatilia halmashauri na ofisi ya wilaya ya Kaskazini ‘B’,aliambiwa amri ya kufungiwa imetolewa na mkuu wa mkoa licha ya kuwa na nyaraka halali za serikali za kumruhusi kufanya biashara hiyo.
Sipano alisema kwa muda mrefu amekuwa na mgogoro wa kimaslahi wa biashara na mwekezaji mmoja jirani yake ambaye amekua hafurahii kitendo cha wageni kutoka katika hoteli yake na kwenda kucheza muziki na kunywa vinywaji katika klabu iliyopo katika hoteli hiyo.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm