9/13/16

IAEA kuanza mchakato wa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya technolojia ya nyuklia kwa nchi za Afrika.


Shirika la nguvu za Atomic duniani(IAEA)limeanza mchakato wa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya technolojia ya nyuklia kwa nchi za afrika ikiwemo tanzania hatua inayolenga kuzijengea uwezo wa kuhakikisha kuwa tahadhari zote za kiusalama zinazingatiwa na teknolojia hiyo inatumika kukuza uchumi na kuondoa umskini kwa wananchi na nchi husika kwa ujumla.
Akizungumza na wawakilishi wa sekta ya mionzi kutoka nchi mbali mbali za afrika waliokutana jijini Arusha Meneja wa Mipango wa shirika hilo Dk,Ugochukwu amesema ili kuhakikisha lengo hilo linatimia wameanzisha mtandao wa mafunzo katika kila nchi utakaorahisisha mawasiliano na utekelezaji wa masuala mbalimbali yanayohusiana na teknolojia hiyo.
 
Mkurugenzi wa usimamizi wa mionzi kutoka tume ya taifa ya mionzi yenye makao yake makuu jijini arusha Dk,Wilboard Muhogora amesema utaratibu wa utekelezaji wa maelekezo ya shirika hilo umeshaanza kufanyiwa kazi na kwamba umekuwa msaada mkubwa  katika jitihada zinazoendelea za kukabiliana na uhaba wa watalam wa teknolojia  ya mionzi unaolikabili taifa.   
 
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazotajwa kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya urenium yanayoweza kutumika kuharakisha maendeleo katika nyanja na miradi mbali mbali ya kiuchumi inayoweza kuwapunguzia wananchi wengi hasa wa vijijini matatizo yanaowakabili yakiwemo ya ukosefu wa huduma bora za afya,maji,miundombinu,na ukosefu wa kipato.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts