Japani yaahidi kuendelea kusaidia kukuza sekta ya elimu nchini Tanzania. | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

9/11/16

Japani yaahidi kuendelea kusaidia kukuza sekta ya elimu nchini Tanzania.


Ubalozi wa Japani nchini umesema utaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kuwa watoto wanaokwama kuendelea na masomo ya Sekondari kutokana na uwezo mdogo wa wazazi na walezi wanapata fursa hiyo.
Ahadi  hiyo inatolewa na Balozi wa nchi hiyo hapa nchini Masaharu Yoshida wakati wa ziara yake katika shule ya sekondari sakura iliyopo wilayami Arumeru ambapo pia anasisitiza umuhimu wa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi.
 
Katika ziara yake hiyo balozi Yoshida amezindua ujenzi wa UKUTA wa shule ambao mkurugenzi wa shule Bi.Frida Mokito anasema ni hatua ya muhimu  katika kuhakikisha usalamawa wanafunzi.
 
Dakta.Batilda Buriani ni balozi mstaafu wa Tanzania nchini Japani anasema licha ya jitihada zawadau katika kuboresha elimu nchini bado changamoto kubwa ni urasimu katika upatikanaji wa visa kwa walimu wanaoingia nchini kujitolea kufundisha.

google+

linkedin