9/23/16

JWTZ lasema liko imara katika kulinda mipaka ya nchi.


Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ  limewahakikishia watanzania kuwa liko imara katika kulinda mipaka ya nchi huku likisema pia kwa sasa limekwisha kujiimarisha  kimfumo na kivifaa  ili kuhakikisha wananchi wake wanakuwa salama nyakati zote.
Kauli hiyo ya JWTZ imetolewa Dar es Salaam na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luten Kanali Venance Mabeyo dakika chache baada ya kufungua mafunzo maalum ya namna vikosi vya JWTZ vitakavyoweza kukabiliana na adui kwenye fukwe  na visiwa vilivyo ndani ya bahari.
 
Mafunzo hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ yameshirikisha vikosi vya anga, nchi kavu na bahari ikiwa ni pamoja na askari wa akiba yanatarajiwa kufikia tamati septemba 30 mjini Bagamoro ambapo Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli atahitimisha mafunzo hayo.
 
Mkuu wa mafunzo kivita Jeshini Meja Jenerali Issa Nassoro amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuwajengea uwezo wapiganaji wa JWTZ hasa katika kipindi hiki ambacho jeshi limejiimarisha kivifaa  huku Kaimu Mkuu wa kamandi ya wanamaji akisema wako imara katika kulinda mipaka yote ya Bahari na kuwataka watanzania kutokuwa na hofu yoyote kwani wako salama.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts