9/10/16

Kamishna TRA akataza simu za mkononiWafanyakazi katika mpaka wa Sirari, mkoani Mara, wanaojihusisha na vitendo vya rushwa, wazembe na wanaofanya kazi kwa mazoea wako hatarini kufutiwa ajira iwapo hawatabadili mwenendo wao wa utendaji.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata ametoa onyo kwa wafanyakazi hao, akiwa ziarani kutembelea ofisi za TRA mkoani Mara na ofisi za forodha zilizopo mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Amesema ofisi hizo zinatia aibu kwa kuendekeza rushwa na kuwaonya watumishi wanaoshirikiana na askari polisi kuvusha magari mpakani bila kulipia kodi na wanaotoa taarifa za siri kuhusu wanaokwenda kuwakamata wafanyabiashara za magendo wanaopitia njia za panya.

“Tunapokea rushwa, tunafanya kazi kizembe na kwa mazoea, tuache tabia hiyo. Kila mmoja ajitathimini kuona kama anastahili kuwa mtumishi wa TRA au la,” amesema.

Kidata amesema anashindwa kuwachukulia hatua moja kwa moja watumishi aliodokezwa wanavujisha siri za mipango ya kukamata magendo na kupokea rushwa kwa kuwa hajawahi kuzungumza nao.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts