9/11/16

Kaya maskini kufadhiliwa masomo UDSM

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa kushirikiana na Kampuni ya Mohamed Enterprises kimeanzisha mfuko wa kudhamini wanafunzi 10 wa elimu ya juu kila mwaka, ambao watakosa mkopo na wanaotoka katika familia masikini.Hatua hiyo imetokana na ukosefu wa mikopo kwa wanafunzi wengi, hususan wanaotoka katika familia masikini na kwamba UDSM na Mo watawasomesha wanafunzi hao bure kwa kipindi cha miaka minne.

Udhamani huo hadi kukamilika kwake, umelenga kuwasomesha wanafunzi 40 na kwamba kila mwaka watakuwa wakisomeshwa wanafunzi 10.

Hayo yalibainishwa juzi na Mkurugenzi wa Shahada za Awali wa UDSM, Profesa Allen Mushi, wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema hatua hiyo itasaidia kuinua ndoto za wanafunzi wengi kutoka familia masikini ambao wanashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu.
 
Zaidi tafuta gazeti la nipashe Leo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts