Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

9/6/16

Kikongwe wa Miaka 87 Atupwa Jela


 
 Kweli duniani kuna mambo na kama huamini basi tembea uyaone. Mkazi mmoja amehukumiwa kifungo cha miezi minane jela na mahakama moja ya nchini Ujerumani kwa kosa la kukanusha tukio la kuuawa umati wa Wayahudi nchini humo, maarufu kama Holocaust.
Shirika la Habari la Ujerumani limeripoti tukio hilo likisema Ursula Haverbeck, mwenye umri wa miaka 87 alikutwa na hatia ya kukanusha kutokea mauaji hayo na Mahakama ya Detmold imeamua kumfunga jela miezi minane.
Akielezea kile alichokiita msimamo wake, Ursula alisema Wayahudi walikuwa wakiishi maisha salama na ya kawaida katika kambi ya Wanazi ya Auschwitz na kamwe hawakuwa wakiadhibiwa bali hiyo ilikuwa ni kambi ya wafanyakazi wa kawaida tu.
Jaji katika mahakama hiyo aliondoa uwezekano wa kikongwe huyo kupewa msamaha kutokana na historia yake ikiwamo kuonyesha dharau kubwa wakati akiwa mahakamani.
Alisema mtuhumiwa huyo amewahi kukutwa na makosa mengi ambayo baadhi yalichukua sura ya uchochezi.
“Mahakama haitarajii Ursula kupewa msamaha wa parole kwa vile ameonyesha dharau kubwa,” alisema.
Mahakama nyingine zimewahi kutoa hukumu dhidi ya Ursual kutokana na kukanusha mauaji hayo yanayodaiwa kufanywa na Wanazi wa Ujerumani dhidi ya Wayahudi.
Ursula amekuwa akitambulika kutokana na misimamo yake mikali na hivi karibuni alimwandikia barua Meya wa Detmold, Rainer Heller akikanusha kuwapo mauaji hayo ambayo yanadaiwa kufanywa wakati wa utawala wa Adolf Hitler.