9/4/16

Kimbunga Vyeti Feki Chazoa Vigogo Kibao

HATIMAYE ile kazi ya kuhakiki vyeti halisi vya elimu na taaluma za watumishi wa wizara na taasisi mbalimbali za umma imeanza kuibua kilio cha aina yake baada ya kubainika uwapo wa watumishi kibao waliojipatia ajira kiujanja-ujanja kwa kutumia vyeti bandia.


Na sasa, matokeo ya kimbunga cha uhakiki huo yameibua pigo la aina yake lililoanza kuwakumba watumishi hao, wakiwamo vigogo wanaoshikilia nafasi mbalimbali za juu katika taasisi na idara mbalimbali za Serikali.

Taarifa ambazo Nipashe ilizipata wiki hii kupitia vyanzo vyake na kisha kuthibitishwa jana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, ni kwamba tayari kuna orodha ya watumishi waliobainika kupata ajira wakitumia vyeti bandia na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea, huku hatua za kisheria na kinidhamu ziko mbioni kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa wote wa udanganyifu huo.

Chanzo: Nipashe
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm