9/11/16

Kuna Ulazima wa Barabara Morogoro-Dodoma Kupanuliwa?

Katibu wa Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua), Frank Mgasa amesema barabara kutoka Morogoro kwenda Dodoma inatakiwa kupanuliwa ili kuepuka msongamano wa magari baada ya Serikali kuhamia mjini hapa.

Akizungumza jana, Mgasa alisema baada ya Serikali kuhamia Dodoma kutakuwa na ongezeko la magari yanayoingia mjini hapa kutoka Dar es Salaam, hivyo ni vyema barabara hiyo ikapanuliwa.

“Barabara ya Morogoro kwenda Dar es Salaam kuipanua hivi sasa ni gharama kubwa kwa kuwa itabidi Serikali iwalipe fidia watu wengi ili kupisha upanuzi lakini kwa Dodoma kwenda Morogoro bado ipo wazi kwa sehemu kubwa, hivyo ni rahisi kuchukua hatua,” alisema.

Kuhusu chama hicho, Mgasa alisema wana ofisi katika kanda sita zinasaidia kutoa huduma kwa abiria wanaopata matatizo mbalimbali.

Hata hivyo, alisema chama hicho kinafanya kazi kwa kujitolea kutokana na kukosa chanzo cha mapato.

Mkazi wa Nzuguni, Mwajuma Mwampambe alishauri chama hicho kufungua ofisi za zaidi mikoani ili kusikiliza malalamiko ya abiria, ikiwamo lugha chafu kutoka kwa makondakta.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts