9/6/16

Lugha ya kichina yashika kasi UDSM
 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimepokea walimu 24 kutoka Chuo cha Zhejiang Normal cha China watakaosambazwa katika baadhi ya shule na vyuo nchini ili kujifunza Kiswahili na kufundisha lugha yao.

Ujio wa walimu hao ni mkakati wa kutimiza lengo la kuboresha ufundishaji wa lugha katika nchi za Tanzania na China zenye historia ya muda mrefu wa ushirikiano.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha walimu hao, Kaimu Makamu Mkuu wa UDSM (Taaluma), Profesa Florens Luoga amesema ili kuitumia fursa iliyopo ya kujifunza Kichina na kukitangaza Kiswahili duniani, kuna kila sababu ya kufurahia ujio wa wanafunzi hao.

Profesa Luoga amesema katika kuhakikisha mafunzo hayo ya lugha yanakuwa endelevu, mwakani UDSM itaanza kutoa shahada ya lugha ya Kichina.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius ya UDSM inayofundisha lugha ya Kichina, Profesa Zhang Xiaozhen amesema baadhi ya wanafunzi hao watakaa Tanzania kwa miaka miwili na wengine mwaka mmoja.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts