Mgogoro waibuka upya kati ya CCM na CHADEMA Karagwe. | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

9/25/16

Mgogoro waibuka upya kati ya CCM na CHADEMA Karagwe.

 Image result for ccm vs chadema

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera imelazimika kuingilia kati mgogoro unaohatarisha uvunjifu wa amani katika kijiji cha Ihembe One uliodumu mwaka mmoja kati ya chama cha Mapinduzi na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wakigombea jengo la ofisi lililojengwa kwa nguvu za wananchi mwaka 1961.
Mgogoro huo umeibuka baada ya uongozi wa serikali ya kijiji kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema kuanzisha ukarabati wa ofisi ya serikali ya kijiji bila idhini ya wamiliki wa jengo hilo hali iliyosababisha vurugu kati ya wafuasi wa chadema na chama cha mapinduzi katika kijiji cha ihembe one kama wanavyobainisha ukweli wa mambo viongozi wa vyama vya siasa ccm na chadema.
 
Kufuatia hali hiyo kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Karagwe Bw.Godfrey Mheluka akiwa na wajumbe wa kamati hiyo wamelazimika kufika kijiji cha Ihembe One kutuliza ghasia na kutoa maelekezo kwa wananchi wafuate sheria,taratibu na kanuni za nchi katika kutekeleza wa miradi ya maendeleo.
 
chanzo: ITV Tanzania

google+

linkedin